KIPI UTATAZAMA KATI YA FAINAL YA FA AU KUTAZAMA HARUSI HII YA KIFALME
Mwanamfalme Prince William atakosa kuhudhuria fainali hiyo ya kesho Jumamosi kwa kuwa ndiyo siku ya harusi ya nduguye Prince Harry.
Prince William atakuwa msimamizi wa harusi ya nduguye huko Windsor kesho Jumamosi.
William amekuwa rais wa FA tangu mwaka 2006 na mara nyingi ndiye hupeana vikombe na medali.
Mjane wa Ray Wilkins Jackie atatoa kombe hilo kwa washindi huko Wembley
"Prince William hatahudhuria fainali ya FA kutokana na majukumu kama msimamizi wa harusu ya ndugu yake," alisema msemaji wa Kensington Palace.
Msemaji wa FA alisema: "Tunawatakia Prince William na wale watafunga ndoa siku njema."
Ray Wilkins ambaye alifariki mwezi uliopita akiwa miaka 61, alishinda kombe la FA kama mchezaji wa Manchester United mwaka 1983 na kufunga wakati wa fainali.
Pia alishinda kombe hilo mara tatu akiwa meneja wa Chelsea.
Mada zinazohusiana
No comments