MASHABIKI YANGA WAUTAKA UONGOZI KUFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi wa kikosi hicho kufanya maamuzi magumu kuhusiana na kikosi chao ambacho kimekuwa hakina mwenendo mzuri katika msimu huu.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Yanga kupoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho katika hatua ya makundi Afrika dhidi ya USM ALger kwa jumla ya mabao 4-0 Jumapili ya wiki iliyopita.
Wapo walioeleza kuwa inabidi Yanga waanze na waliotia mgomo kuisaliti timu ilipoelekea Algeria kwa ajili ya mchezo huo wa juzi Jumapili.
Mashabiki hao baadhi wameeleza Yanga inabidi ikisafishe kikosi upya ikiwemo kuwapunguza wakongwe na kuwa na damu changa ambayo inaweza kutia morali kwenye kikosi ili kiweze kufanya vizuri.
Vilevile wachezaji wote wanaoonekana kuwa ni mizigo ndani ya timu wafanyiwe mpango wa kuondoshwa wakieleza kuwa hawana msaada wowote ndani ya Yanga.
Licha ya kutaka kusafisha kikosi, wapo pia waliokipongeza kikosi hocho licha ya kupoteza huku wakiwapa matumaini wachezaji kuchukulia matokeo hayo kama sehemu ya mchezo wa siku zote katika mpira.
No comments