MO RASHID RAMS ASAJILIWA SIMBA SC
Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya, Mohamed Rashid ‘ Mo’ na kumsainisha mkataba wa miaka mitatu.
Usajili huo wa Mohamed Rashid aliyemaliza na mabao 10 ya VPL 2017/18, unakuwa usajili wa tatu kukamilika msimu huu baada ya Adam Salamba na Marcel Kaheza kujiunga na mabingwa bao huku wote wakiwa mshambuliaji.
Mohammed Rashid sasa ataungana na washambuliaji wenzake ambani ni kinara wa mabao msimu ulioisha wa 2017/18, Emmanuel Okwi akimaliza na mabao 20, John Bocco aliyemaliza na mabao 14, Marcel Kaheza aliyemaliza na mabao 14 pamoja na Adam Salamba aliyemaliza na mabao 8, kuiongoza Simba katika michuano yote ijao katika msimu wa 2018/19.
Baada ya kukamikisha usajili huo sasa ni rasmi Simba wameachana na mshambuliaji wao Mrundi Laudit Mavugo mashabiki wa Simba wakipendelea kumwita ‘King Lodie Mavugo’, mwingine ni Juma Luizio ‘Ndanda’ wachezaji hao wote wanaachwa baada ya mikataba yao kuisha.
Pia imefahamika kuwa mabingwa hao wa VPL 2017/18 wamepanga kumpeleka kwa mkopo mshambuliaji wao kinda aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili Moses Kitandu.
No comments