USAJILI WA SINGIDA UNITED WAWEKWA HADHARANI
Klabu ya Singida United yenye makazi yake Mjini Singida imefanikiwa kuinasa saini winga chipukizi wa Ndada Fc ya Mtwara Tiba John George ambapo ametambuliswa rasmi leo na kusaini naye mkataba wa miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amemtambulisha mchezaji huyo mbele ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Hotel ya Naura Springs, jijini Arusha leo.
Yanga nao walikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zinamuwania winga huyo kabla ya kuachana nae na kuamua kumrejesha Mrisho Khalfani Ngassa ‘Anko’.
Mbali na Tiber, Singida United imewatambulisha wachezaji wengine wawili waliowasajili, ambao ni Felipe Olveira do Santos raia wa Brazil na Amara Diaby, raia wa Ivory Coast.
Wachezaji hao wote watakuwa sehemu ya kikosi cha Singida katika michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza June 03 hadi June 10 mwaka huu nchini, Kenya.
No comments