Breaking News

SABABU ZA UWANJA WA BUNJU KUSIMAMA HIZI HAPA

Uongozi wa Mabingwa wapya msimu huu wa 2017/18 Simba Sc, kupitia Haji Manara, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, amefafanua kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wao uliopo Bunju, Jijini Dar es Salaam, kusimama.


Manara ametaja sababu ya mwendelezo wa Uwanja huo kutoendelea ni kutokana sakata la viongozi wao wa juu,ambao ni Rais wa Simba, Evans Aveva pamoja na Makamu Nyange Kaburu kuwa mahakamani.


Akiongea na EFM Manara ameyasema hapo kutokana na maswali mbalimbali ambayo yamekuwa yakiulizwa na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kutaka kujua ujenzi wa Uwanja huo umefikia wapi.


Ikumbukwe Simba walianza harakati za ujenzi wa Uwanja huo mwaka jana lakini baadaye viongozi hao tajwa hapo juu walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo Dar es Salaam kwa makosa ya utakatishaji fedha kiasi cha dola 300,000 ambazo ni sawa na milioni 700 za Kitanzania


No comments