TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA MAY31, 2018
Manchester United wanataka kusaini mkataba mchezaji wa safu ya mashambulizi wa kikosi cha West Marko Arnautovic - the Hammers wanataka mlipo ya pauni £50m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Australia. (Sky Sports)
Lakini West Ham inasema hawataki kumuuza mshambuliaji huyo msimu huu . (Evening Standard)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alionekana katika mchezo wa kirafiki Jumatano baina ya Austria na Urusi , mchezo ambao aliucheza Arnautovic. (Vivaro News)
Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji kutoka Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29 baada ya kutangaza kuwa anataka kuondoka Bayern Munich. (Mirror)
Liverpool inataka kumuuza mshambuliaji wao Mfaransa Nabil Fekir mwenye umri wa miaka 24 kwa Lyon kwa euro milioni 60m (Le Parisien)
Na the Reds wanae mlindalango wa Barcelona Jasper Cillessen raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 kwenye orodha yake ya wachezaji wake. (Mundo Deportivo)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Italia Jorginho, mwenye umri wa miaka 26, yuko tayari kujiunga na kikosi cha Manchester City kutoka Napoli baada ya kununuliwa kwa euro milioni hamsini 50m baaada ya kukubali mkataba wa miaka mitano na Man city . (La Gazzetta dello Sport - in Italian)
Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemshauri mshambuliaji wa safu ya mbele Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 27, aendelee kubaki Atletico Madrid badala ya kujiunga na Barcelona. (RMC Sport- in French)
'Wachezaji wa Uingereza wazungumzia ubaguzi wa rangi Urusi'
Arsenal wamekamilisha mipango ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati ya Ufaransa Yacine Adli mwenye umri wa miaka 17 kutoka kikosi cha Paris St-Germain. (Mirror)
Mshindi wa Kombe la Dunia la Brazil Ronaldo anataka kununua klabu ya Uhispania Real Valladolidkwa euro milioni 30 . (O Globo - in Portuguese)
No comments