Breaking News

KIKOSI CHA YANGA KINACHOELEKEA NAIROBI KWENYE MASHINDANO YA SPORTPESA

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup, inayotarajiwa kuanza June 03 hadi June 10 ikizihusisha timu nane huku 4 zikitoka Tanzania na 4 za Kenya.

Timu zote zinazoshiriki michuano hii ni zile zinazodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa ambapo kwa Tanzania ni Simba, Yanga, Singida United na JKU ya Zanzibar.

Katika michuao hiyo inayoanza June 03 katika hatua ya mtoano, Bingwa atajinyakulia kitita cha Milioni 68 pamoja na kupata nafasi ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton inayoshiriki ligi kuu nchini humo ya EPL, huku mchezo huo ukitarajiwa kufanyika kwenye dimba la Goodison Park.

Hiki hapa kikosi kamili kilichoondoka leo asubuhi na mapema

Youthe Rostand Jehu, Ramadhan Kabwili, Hassan Ramadhan Kessy, Buruan Yahaya Akilimali, Mwinyi Haji Ngwali, Pius Charles Buswita, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pato Ngonyani, Ibrahim Ajib Migomba na Maka Edward.

Wengine ni Yohana Mkomola, Thabani Scara Kamusoko, Matheo Anthony, Amissi Tambwe, Juma Hassan Mahadhi, Said Juma Makapu, Said Mussa Bakari, Papy Kabamba ‘Tshishimbi’, Yussuf Mhilu na Raphael Daudi Loth.

No comments