Breaking News

TETESI ZA USAJILI NDANI YA SIMBA SC

Taarifa zinaeleza kuwa kipa nambari mbili wa Simba Sc, Said Mohammed ‘Nduda’ yuko mbioni kutemwa na timu hiyo kutokana na kutokuwa na msaada katika kikosi hicho msimu huu.


‘Nduda’ alitua msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar, lakini alishindwa kuisaidia timu yake hiyo kutokana na kuandamwa na majeraha kwa kipindi kirefu.


‘Nduda’ ameidakia Simba katika mchezo mmoja tu wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar May 19 na kufungwa bao 1-0, bao lililovunja rekodi ya Simba ya kutofungwa msimu huu ambapo ilicheza michezo 28 bila kupoteza hata mmoja.


Kwingineko imeripotiwa kuwa mchambuliaji wa Majimaji Fc ya Ruvuma mwenye mabao 13 msimu huu Marcel Bonaventure Kaheza yuko mbioni kujiunga na mabingwa hao wapya msimu huu.


Katika hatua hiyo ya usajili pia klabu za Singida United na Azam Fc zinatajwa kumuwania nyota huyo anayefanya vizuri katika safu ya ushambuliaji ya Majimaji Fc.


Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Mrundi Laudit Mavugo naye pia yuko mbioni kuondoka Simba Sc baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu.


Pia klabu hiyo ya Simba Sc huenda ikumtupia vilango beki wake Salim Mbonde hii ni kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara, ambapo naye ameshindwa kuitumikia klabu hiyo msimu huu.


Baada ya Shiza Kichuya kutajwa kutimkia TP Mazembe kutokana na Baba Mzazi kutaka awe katika level za Samatta na Msuva, Mama mlezi wa nyota huyo wa Simba amesema kokote tu aende maana mpira ndio maisha ya Kichuya toka akiwa Primary.


Baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu kutokana na mejeraha ya mara kwa mara, Haruna Niyonzima imesemekana kuwa ataendelea kuitumikia Simba kwani bado ni mchezaji muhumu sana kwa msimu ujao.


Aidha wachezaji wa kimataifa ambao wana asilimia kubwa ya kuachwa katika kikosi hicho kutokana na mapendekezo ya viongozi ni beki Mganda Juuko Murishid na washambuliaji Laudit Mavugo (Burundi) na Mghana Nicholaus Gyan.


No comments