VIINGILIO MECHI YA (ASFC) KATI YA MTIBWA DHIDI YA SINGIDA HIVI HAPA
Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kupigwa June 02 mwaka huu mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kueleka Fainali hiyo kiingilio cha chini kitakuwa buku tu, lengo kuu la kuweka kingilio hicho kwa ajili ya kuwavutia mashabiki wengi zaidi kupata nafasi ya kuona mchezo huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Peter Temu amesema, TFF imewataarifu kuwa viingilio vya mchezo huo vimegawanywa katika makundi matatu kulingana na uwanja huo ulivyo.
Ambapo kwa jukwaa kuu kiingilio kitakuwa Tsh, elfu 10,000 tu na jukwaa (B1) na (B2) itakuwa Tsh, shilingi 2,000) huku jukwaa (C)ambalo ndilo mzunguko kiingilio kitakuwa sawa na bure kabisa ambacho ni Tsh, elfu 1,000.
“Kiingilio hiki ni pendekezo la kamati ya ARFA iliyokutana wiki iliyopita na tuliwakilisha TFF hivyo tunashukuru uongozi TFF kwa kukubali mapendekezo yetu” amesema Temu.
Amesema, kwa kuwa tiketi za mchezo huo bado hazijawasili ni ngumu kueleza zitaanza kuuzwa lini japo alihaidi zitaanza kuuzwa siku moja hata kabla ya mchezo huo ikiwa ni kutoa fulsa kwa wale wanaoishi mbali hasa wapenzi wa timu ya Singida na Mtibwa.
No comments