Breaking News

KIPA YANGA AMTETEA ROSTAND NA KUWAPONDA MABEKI






Baada ya Mcameroon, Youthe Rostand kupokea lawama nyingi kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa Yanga juu ya ubora wake golini, kipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter, ameibuka na kumtetea.

Manyika amesema kitendo cha mashabiki wengi wa Yanga kumtupia lawama Rostand hakina maana yoyote kutokana na kipa huyo kuonesha ubora stahiki uwanjani.

Manyika ameeleza anaamini Rostand ni kipa bora hivyo wale wote wanaomkosoa hawako sahihi na badala yake wazidi kumvunja nguvu za kuendelea kuitendea haki nafasi yake kwenye goli.

Kipa huyo ambaye aliwahi kutamba na Yanga miaka ya nyuma amewatupia lawama mabeki wa Yanga kutokana na kiwango walichoonesha akisema walisababisha Rostand kufungwa na si yeye kufanya makosa.

Manyika amesema mabeki wa Yanga na kikiso kizima kwa ujumla kiliwa na mapungufu mengi kitu ambacho kimepelekea timu kufungwa mechi mbili mfululizo huku akieleza mfumo ambao ulikuwa unatumika ulikuwa haueleweki.

Kufungwa kwa Yanga juzi na Gor Mahia kwa mabao 3-2 kumewafanya waendelee kuwa mkiani kunako kundi D wakiwa na alama moja pekee ambayo waliipata baada ya suluhu ya 0-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

No comments