Breaking News

HII HAPA OFA YA CLUB YA SIMBA SC KWA MASHABIKI WAKE


Simba imeandaa mkakati wa kusafirisha mashabiki wake kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kupata hamasa katika mchezo wao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Fc, mchezo utakaochezwa Desemba 15 mwaka huu, Mjini Kitwe

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kwa kutambua mchango wa mashabiki wao, wameweka gharama rafiki kwa watakaopenda kusafiri na timu kwa kuchangia kiasi cha shilingi 130,000 kwa safari ya kwenda na kurudi.

“Tumeamua kuandaa mkakati huu kwa ajili ya mashabiki wetu, mwisho wa kujiandikisha kwa anayehitaji kusafiri na timu ni Jumanne jioni na pia ufanyaji wa malipo ufanyike kwa mawasiliano ya Jacob Gamaly msaidizi wangu kwa namba zifuatazo 0659 929420,0766 051826, ” amesema Manara.

Aidha Manara amesema gari ya mashabiki itaondoka Dar es Salaam Alfajiri siku ya Alhamisi na kufika Kitwe Ijumaa jioni. Kila msafiri anatakiwa awe na nauli kamili na fedha za kujikimu akiwa huko, pamoja na hati ya kusafiria inayokidhi matakwa ya kisheria na hati ya chanjo.

Mchezo wa marudiano utapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Desemba 23, ambapo mshindi wa jumla atakata tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

No comments