TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO
Barcelona wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hawamuuzi kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez, 25, kwa Arsenal mwezi huu. (Mirror)
Wolves wamekamilisha mpango wa kumchukua Tammy Abraham kutoka kwa klabu yake ya Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 21 anatarajiwa sasa kufanya uamuzi leo Jumatatu kuhusu iwpao atakatisha mkopo wake Aston Villa na kwenda Molineux. (Express and Star)
Manchester United wanamfuatilia kwa karibu beki wa AS Roma kutoka Ugiriki Kostas Manolas, 27, ambaye ana kifungu cha £32m cha kumfungua kutoka kwenye mkataba wake. (Sun)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba haiwezekano kwa winga raia wa England Phil Foden mwenye miaka 18 kuondoka klabu hiyo kwa mkopo. (Independent)
Arsenal hawatarajiwi kuwasili ofa nyingine kumtaka winga wa AS Roma Cengiz Under ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m baada ya ofa yao ya awali ya £35m ya kumtaka mchezaji huyo wa Uturuki mwenye miaka 21 kukataliwa. (Star)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema hajapokeza taarifa zozote kumhusu mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja - licha ya klabu yake kuhusishwa na ununuzi wa mchezaji huyo wa miaka 20 kutoka England mwezi huu. (Mirror)
Abdulkadir Omur, 19, kiungo wa kati Mturuki anayechezea Trabzonspor ambaye amehusishwa na Liverpool amesema anaweza kufurahia sana fursa ya kujiunga na klabu hiyo ya meneja Jurgen Klopp. (Liverpool Echo)
Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafael Benitez bado hajashiriki mazungumzo yoyote na klabu hiyo kuhusu kuongeza mkataba wake licha ya taarifa kwamba klabu hiyo ilipendekeza kumpa mkataba mwingine wa mwaka mmoja hivi majuzi. (Newcastle Chronicle)
Meneja Eddie Howe anasema Bournemouth huenda wakawanunua wachezaji zaidi mwezi huu hata baada ya kuwachukua Dominic Solanke na Nathaniel Clyne. (Sky Sports)
Nathaniel Clyne Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Clyne alihamia Bournemouth siku moja na Dominic Solanke
Barnsley huenda wakawasilisha nia ya kumtaka mshambuliaji wa England mwenye miaka 21 anayechezea Sunderland Andrew Nelson, ambaye amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Darlington inayocheza Ligi ya Taifa ya Kaskazini. (Sunderland Echo)
Nathaniel Clyne Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nathaniel Clyne akichezea Liverpool
Hibernian wamemfanyia majaribio kipa wa Tottenham Tom Glover na kumpeleka mchezaji huyo wa Australia wa miaka 21 kwenye kambi yao ya majira ya baridi jijini. (Edinburgh News
No comments