TETESI ZA USAJILI LEO BARANI ULAYA
Chelsea inatarajiwa kuwasilisha dau la £50m kumunua mshambuliaji wa Paris St Germain na Uruguay Edinson Cavani, 31. (Sunday Express)
Arsenal imeanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez na wanamatumiani makubwa ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Observer)
Denis Suarez
Lakini ,mkufunzi wa Gunners Unai Emery pia anataka kumsaini beki na winga . (Mail on Sunday)
Fulham inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi na wamejiandaa kutoa £15m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Ubelgiji. (Sun on Sunday)
Divock Origi
Bournemouth itapinga maombi yoyote kutoka Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 26. (Sunday Mirror)
Chelsea itakosa huduma za kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 31 Cesc Fabregas, ambaye ni mmojawapo wa wachezaji bora kucheza nchini Uingereza kwa miaka mingi, kulingana na beki wa Brazil David Luiz.
Mchezaji huyo wa Uhispania anatarajiwa kujiunga na klabu ya Ufaransa Monaco.(Talksport)
Cesc fabregas
Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho amekataa kazi ya kuifunza Benfica baada ya klabu hiyo ya Ureno kumfuta kazi kocha wake Rui Vitoria wiki hii. (Record - in Portuguese)
Mkufunzi mwengine wa United wa zamani David Moyes, ana hamu ya kutaka kuifunza klabu ya Stoke City (Daily Star Sunday)
Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich angekuwa ameinunua Arsenal badala ya Chelsea miaka 16 iliopita lakini akaelezewa kimakosa kwamba klabu hiyo ilikuwa haiuzwi wakati huo na benki ya Uswizi.. (Sun on Sunday)
Jose Mourinho
Inter Milan wamefanya mazungumzo na klabu ya Sampdoria kuhusu beki wa Denmark mwenye umri wa miaka 22 Joachim Andersen, ambaye amehusishwa na Tottenham.. (Corriere dello Sport, via Inside Futbol)
West Ham ina mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan Antonio Candreva, 31. (Corriere dello Sport - in Italian)
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone anasema kuwa ana mpangowa kumzuia beki wa Uruguay mwenye umri wa miaka 32 Diego Godin, ambaye analengwa na Man United katika klabu hiyo ya Uhispania.. (Sunday Express).
Hector Bellerin
Beki wa Arsenal mwenye umri wa miaka 23 Hector Bellerin , ambaye anauguza jeraha siku ya Jumamosi alihudhuria maonyesha ya London fashion Week badala ya kutazama timu yake ikicheza dhidi ya Blackpool katika kombe la FA. (Mail on Sunday)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amewataka wafanyikazi wake kupata funzo la kujua kutumia kamera za ndege zisozokuwa na rubani ili kumwezesha kupata mitazamo tofauti wakati wa mazoezi.. (Sun on Sunday)
imefanya mkakati wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham, Mousa Dembele, 31. (Sky Sports)
Mchezaji wa Barcelona Denis Suarez, 24, anakaribia kujiunga na Arsenal.
Mchezaji huyo wa Uhispania awali alikuwa amehusishwa na Everton pamoja na West Ham. (Sport - in Spanish)
Haki miliki ya picha Getty Images
Meneja wa Unai Emery inaitaka Arsenal kuendelea kuwa na Aaron Ramsey mpaka mwisho wa msimu badala ya kiungo wa kati wa Wales ambaye amekuwa akihusishwa na Juventus, kuondoka mwezi huu. (London Evening Standard)
Bosi wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Peter Kenyon bado yuko katika ushindani wa kuinunua Newcastle na tayari amewasiliana na mmiliki Mike Ashley na kuhaidiana kuwa watafanya mazungumzo tena mwezi huu. (Mail)
Kenyon anaamini kuwa mmiliki wa Newcastle yako katika hatua ya juu yenye matumanini. (Newcastle Chronicle)
Liverpool haitamruhusu kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 30 kuondoka kwa mkopo mwezi huu. (Sky Sports)
Fenerbahce ilitoa kiwango kikubwa cha mkopo kwa mchezaji huyo wa zamani wa Southampton, Lallana mpaka mwisho wa msimu. (Fotomac, via Express)
Manchester City imeshindwa kumsajili mchezaji wa Toulouse Jean-Clair Todibo, ambaye sasa hivi anatarajia kuhamia Barcelona. (Independent)
Haki miliki ya picha Getty Images
Mlinzi wa West Ham Reece Oxford, 20, amehusishwa kuhamia Borussia Monchengladbach mwezi huu, ingawa anaweza kusubiri msimu wa kiangazi ili ahamie Arsenal. (Mirror)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amehusishwa na kuhamia Villarreal, jambo ambalo anaweza kulitimiza akiwa amerudi katika nchi yake.
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot atajiunga na Barcelona bila malipo yeyote katika kipindi hiki cha kiangazi.
Tottenham imeongeza nafasi ya kumpoteza mlinzi wa kati, Toby Alderweireld, 29, baada ya kuondoa kifungu kilichokuwa kinatoa Euro milioni 25 licha ya kuongeza mkataba wake. (ESPN)
Vicente Iborra anaweza asirudi Leicester baada ya kupewa muda wa kupumzika na kurejea Uhispania kwa ajili ya familia yake.
Bosi wa West Ham, Manuel Pellegrini amekataa mapendekezo yaliyotolewa na mshambuliaji Andy Carroll na Marko Arnautovic,ambapo wote wanaweza kuondoka katika mwezi huu. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja, 20 amehusishwa na Tottenham, Manchester City na Southampton, kukataa mkataba mpya na Black Cats. (Talksport)
Mchezaji wa Aston Villa Ross McCormack, 32, anakaribia kurudi katika klabu yake ya zamani ya Motherwell kwa mkopo. (Birmingham Mail)
Torino inajiandaa kumpa mchezaji Watford ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumzuia mchezaji wa kimataifa wa Argentina Roberto Pereyra, 27,asiondoke kipindi cha kiangazi . (Tuttosport, via Inside Futbol)
Munir El Haddadi, 23 amekataa nafasi ya kuongeza mkataba wake Barcelona na sasa anajiandaa kuondoka bila malipo msimu wa kiangazi. (ESPN)
No comments