Breaking News

HIZI HAPA KUSHUKA DIMBANI LEO SPORTPESA CUP


By Godfrey godstar,

LEO Uwanja wa Taifa kutakuwa na michezo miwili ya SportPesa Cup ambapo timu nne zitamenyana kutafuta mshindi atakayetinga hatua ya nusu fainali.

Mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali Uwanja wa Taifa utakuwa kati ya Mbao na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi majira ya saa 8:00 mchana.

Jioni saa 10:00 kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba na AFC Leopards ikiwa ni hatua ya robo fainali.

Timu kutoka Tanzania kwa sasa zimebaki mbili tu ambazo zitacheza leo Simba na Mbao, mbili tayari zimetolewa hatua ya robo fainali ambazo ni Yanga na Singida United.

No comments