JUMA ABDUL WA YANGA AWAPA MBINU MPYA SIMBASC LEO
Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Abdul amesema kuwa kikosi cha Simba kitakutana na upinzani kwa waarabu kutokana na namna walivyo na kasi katika ushambuliaji hivyo wanapaswa kuwa makini.
Abdul amesema kuwa michezo ya kimataifa huwa inakuwa na ushindani mkubwa hasa kutokana na kila timu kujipanga vizuri hivyo asili ya waarabu wengi wanapenda kutumia viungo na mashambulizi ya kasi.
"Waarabu muda wote wakiwa nyumbani ama ugenini hupenda kushambulia kwa kasi na kutumia viungo wao katika kutengeneza mashambulizi hivyo Simba wanapaswa wawe makini.
"Ubovu wao mara nyingi huwa sehemu ya ulinzi ila inabebwa sana na kufichwa na viungo wao sasa ili waweze kupata matokeo inabidi walazimishe kupata matokeo mapema na wawe imara kwa upande wa ulinzi, nina imani watafanya vizuri wakijipanga," alisema Abdul.
Simba wapo Kundi D katika Ligi ya Mabingwa ambalo lina timu kama JS Saora ya Algeria, Al Ahy ya Misri na AS Vita ya Congo leo wataanza kazu dhidi ya JS Saoura Uwanja wa Taifa.
No comments