Breaking News

KWA HILI LAZIMA UFANISI UONGEZEKE NDANI YA KIKOSI CHA SIMBASC

Uongozi wa klabu ya Simba katika kuogeza ufanisi wa timu umemteua Ndg. Patrick Rweymamu kuwa meneja wa muda wa timu ya Simba, huku Ndg. Abbas Ally akiendelea na majukumu yake ya awali ya kuwa mratibu wa timu.

Wakati huohuo kikosi cha wachezaji ishirini (20) na benchi la ufundi wakiambatana na viongozi kadhaa wataondoka kesho jioni January 29, 2019 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kucheza mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly.

Simba itaondoka kwa shirika la ndege la Ethiopia kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia na kisha kuelekea mjini Alexandria, Misri ambapo mchezo huo unatarajia kuchezwa siku ya Jumamosi February 2, 2019.

No comments