Breaking News

MBANA SAMATTA HAKAMATIKI

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta, msimu huu ameonekana kudhamiria kufanya makubwa zaidi katika Klabu yake hiyo kutokana na kuisaidia kupata matokeo katika michezo muhimu kwa klabu hiyo.

Katika mchezo wa Derby wa jana ugenini dhidi ya Sinti Truiden Samatta aliisaidia Genk kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, huku akifunga bao moja na kutoa assist ya bao moja.

Ushindi huo unaifanya KRC Genk iongoze Ligi kwa kuwa na jumla ya ponti 51 wakifuatiwa na Club Brugge waliopo nafasi ya pili wakiwa na point 41.

Bao la Samatta katika mchezo huo linakuwa bao lake la 16 la Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji msimu huu akifuatiwa na Landry Dimata wa Anderletch mwenye mabao 13.

No comments