Breaking News

MSIKILIZE ADAM SALAMBA KUHUSIANA NA MAPINDUZI

Kikosi cha Simba ambacho kinatarajiwa kuondoka kesho Jumatano kwenda Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi, kinakabiliwa na michuano migumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo
wamepangwa Kundi D pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, JS Saouro ya Algeria na AS Vita Club ya Congo DRC. Makundi yapo manne na timu 2, za mwanzo kutoka kila kundi zitapata nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Dar es Salaam. Straika wa Simba, Adam Salamba amesema anataka mwaka 2019, uwe wa mafanikio kwake na amejipanga kutumia vizuri nafasi ambayo ataipata katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Salamba ambaye amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Lipuli FC ya Iringa, amesema michuano hiyo ina faida kubwa kwake.

"Mwaka 2019, nataka uwe wangu wa mafanikio nikianza na mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Nina malengo ya kufika mbali kwenye soka na ipo siku moja nitakuwa anga nyingine kama ilivyo kwa kina Mbwana Samatta ambao wanaiwakilisha Tanzania kwa mataifa mengine,"alisema Salamba.

Akizungumzia kikosi chake cha Simba, Salamba anasema licha ya kudondosha tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mwakani baada ya kutolewa na klabu ndogo ya Mashujaa hatua za awali anaamini wana nafasi kubwa ya kuonyesha uwezo wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
"Tunatakiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hilo ndiyo jambo la kwanza baada ya kuondolewa FA. Pia, kuweka nguvu zaidi kwenye Ligi ya mabingwa Afrika hasa katika nafasi hii tulipo pamoja na Kombe la Mapinduzi,"alisema Salamba.

No comments