SIMBA WANA BALAA HUKO ZAZIBAR, WAWATUMIA MASHABIKI UJUMBE HUU
LICHA ya kupata ushindi katika mchezo wao wa jana wa kombe la Mapindizi dhidi ya Chipukizi uliochezwa Uwanja wa Amaan, uongozi wa Simba umewaomba radhi mashabiki kwa kushindwa kuwapa burudani kubwa.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema walikuwa na kikosi kizima ambacho waliamini kingefanikiwa kupata ushindi mnene badala yake wamepata ushindi mwembamba.
"Tuliwaahidi furaha na soka maridhawa watu wa Zanzibar na wale walioangalia kupitia Azam TV, bila shaka mmeridhika ila tunawaomba radhi kwa ushindi 'Mwembamba wa goli 4-1' tulioupata," alisema Manara.
Kwenye ushindi huo wa jana, Meddie Kagere alifunga mabao mawili dakika ya 33 na 59, Nicolous Gyan alifunga dakika ya 55 na John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 83 na kuifanya Simba kufanikiwa kushinda kwa mabao 4-1.
Bao la kufutia machozi kwa Chipukizi lilifungwa na Evance Godwin ambaye alifunga bao maridadi sana akiwa kwenye eneo la 18 lililomshinda Ally Salim.
No comments