TIMU ZA TANZANIA ZINAKOSEA WAP SPORTSPESA
Kwa mara ya tatu mfululizo kombe la SportPesa linakwenda Kenya baada ya vilabu vya Tanzania kushindwa kufua dafu mbele ya vilabu vya Kenya.
Hii ni mara ya pili michuano ya SportPesa inafanyika Tanzania lakini bado vilabu vya nyumbani vimeshindwa kufanya vizuri na kuishia kuwa wasindikizaji.
Mashindano hayo ambayo yanashirikisha vilabu vilivyodhaminiwa na SportPesa na vilabu vingine ambavyo hualikwa, msimu huu amepatikana bingwa mpya Kariobangi Sharks ikiwa ni baada ya Gor Mahia kushinda kombe hilo mara mbili mfululizo katika misimu miwili iliyopita.
Baada ya Simba, Yanga, Mbao na Singida United kushindwa kuwa mabingwa wa SportPesa Cup, zimeshindwa kuingiza zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania ambazo bingwa wa michuano hiyo anapata ndani ya siku sita (6).
Vilabu vya Tanzania kwa mara nyingine vimepoteza fursa ya kucheza na Everton inayoshiriki ligi ya England.
Ukifanya uchambuzi wa kawaida ndani ya miaka mitatu ya mashindano haya haihitaji uwe umeingia daasani ili kubaini kwamba timu za Kenya zimetuzidi.
No comments