Breaking News

WOLVERHAMPTON NI HATARI KWA LIVERPOOL



Mchezaji Ruben Neves alifunga bao la pili kwa ustadi mkubwa na kuwawezesha Wolves kuwatoa nje vinara wa Ligi Kuu ya England kwa sasa Liverpool kutoka kwenye Kombe la FA, kwa kuwalaza 2-1

Wolves wamekuwa wakiwaangusha miamba hata kwenye Ligi ya Premia msimu huu. Wametoka sare na Manchester City, Manchester United na Arsenal na wakawalaza Chelsea na Spurs. Kati ya klabu "sita kuu", ni Liverpool pekee ambao hawajapoteza pointi EPL mikononi mwa Wolves msimu huu.

Liverpool walikuwa wamewachezea wachezaji watatu ambao bado hawajatimiza miaka 18, ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kuchezeshwa kwenye kikosi cha kuanza mechi.

Meneja Jurgen Klopp alikuwa amefanya mabadiliko tisa kwenye kikosi chake cha kawaida cha kuanza mechi, ambapo ndani yake aliwaingiza Curtis Jones, 17, na Rafael Camacho, 18.

Kulikuwa pia na kinda Mholanzi Ki-Jana Hoever aliyejiunga nao baadaye- aliyechezeshwa akiwa na miaka 16, na kuwa mchezaji wa tatu wa umri mdogo zaidi kuwahi kuchezeshwa na klabu hiyo katika mechi ya ushindani.

Aliingizwa uwanjani dakika ya sita baada ya Dejan Lovren kuumia.

Wolves walikuwa wametatizika kupenya ngome ya Liverpool hadi pale dakika ya 38 Raul Jimenez alipowafungulia ukurasa wa mabao kupitia kiungo wa kati James Milner.

Divock Origi aliwasawazishia wageni hao dakika sita baada ya kipindi cha pili kuanza, katika kombora la kwanza la Liverpool lililolenga goli. Kombora lake lilipita katikati mwa miguu ya Leander Dendoncker na kisha kumbwaga kipa John Ruddy.

Lakini mambo ya kutoshana nguvu yalidumu dakika nne pekee, kwani Neves alitoa kiki kali akiwa hatua 31 kutoka kwenye lango, na kombora lake likambwaga kipa Simon Mignolet karibu na mlingoti na mpira ukatulia wavuni dakika ya 55.

Xherdan Shaqiri alipiga frikiki baadaye lakini kipa kuwa amepiga John Ruddy akafanikiwa kuuzuia mpira. Hiyo ilikuwa fursa pekee nzuri nyingine ambayo Liverpool waliipata mechi hiyo.

Wolves, waliowatoa Liverpool nje ya Kombe la FA mara ya pili sasa katika misimu mitatu watakuwa wageni wa mshindi kati ya Stoke na Shrewsbury katika raundi ya nne.

Klopp aliwaingiza Salah na Firmino uwanjani zikiwa zimesalia dakika 20, lakina hawakuweza kuwafaa majogoo hao wa Anfield.
Divock Origi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Divock Origi alikuwa anachezea Liverpool mara ya nne pekee msimu huu, na ilikuwa mara yake ya pili pekee kuchezeshwa kikosi cha kuanza mechi

"Muhimu zaidi ni iwapo umekomaa, na si umri wako," alisema meneja Jurgen Klopp kumhusu Ki-Jana Hoever baada ya mechi.
Ki Jana Hoever Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ki-Jana Hoever, alijiunga na Liverpool kutoka Ajax mwanzo wa msimu. Alizaliwa Januari 2002
Mambo muhimu

    Wolves walijipatia ushindi wao wa kwanza dhidi ya Liverpool nyumbani katika mechi saba za karibuni zaidi (Sare 3 Kushindwa 3), tangu ushindi wao wa 1-0 mwezi Agosti 1981.
    Liverpool wametolewa nje ya Kombe la FA katika mechi sita kati ya nane za karibuni zaidi walizopangwa na klabu inayocheza Ligi ya Premia.
    Wolves wamewatoa Liverpool kutoka kwenye Kombe la FA mara tano sasa - Stoke ndio pekee ambayo wameitupa nje mara nyingi zaidi shindano hilo (mara sita).
    Bao la Jimenez alilowafungia Wolves lilikuwa lao la kwanza nyumbani dhidi ya Liverpool katika dakika 398 tangu Kenny Miller alipowafunga dakika ya 90 mechi dhidi yao Januari 2004.
    Mabao manane kati ya tisa aliyoyafunga Neves akichezea Wolves mashindano yote ameyafunga kwa makombora ya nje ya eneo la hatari, bao hilo lake jingine alilifunga kupitia mkwaju wa penalti.
    Origi alifunga bao lake la pili Kombe la FA. Lake la kwanza pia alilifunga dhidi ya Wolves Januari 2017.
    Akiwa na miaka 16 na siku 354 days, Hoever amekuwa mchezaji wa umri mdogo zaidi wa Liverpool kucheza FA, na wa tatu kwa jumla kuwachezea mechi za ushindani.
    Shaqiri amekuwa kwenye timu inayoshindwa mechi zake zote nne alizocheza Kombe la FA (tatu akiwa na Stoke).

Nini kinafuata?

Liverpool watakuwa ugenini dhidi ya Brighton Ligi ya Premia Jummaosi, nao Wolves wawe wageni wa Manchester City Jumatatu.

No comments