ADAM SALAMBA ARIPOTI KAMBINI KENYA
-Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Sc, Adam Salamba tayari ameisha ripoti kambini nchini Kenya kwa ajili ya michuano ya Sportpesa inayoendelea Kenya.
-Simba Sc ambayo ilikuwa na wachezaji 17 ambao walifanikiwa kushinda mchezo wa robo fainali kwa kuwafunga Kariobangi Sharks kwa penati (3-2) na kesho watacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kakamega Home Boyz majira ya saa 7 mchana.
-Wachezaji wa Simba ambao wapo Kenya ni magolikipa Aishi Manula na Ally Salim, Mabeki Ally Shomary, Shomary Kapombe, Mohamed Hussein, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, na Paul Bukaba
-Viungo ni Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Juma Rashid na Haruna Niyonzima washambuliaji ni Moses Kitandu, Marcel Kaheza, Mohamed Rashid na Adam Salamba.
No comments