Kisa Asante Kwasi Yondani aigomea Kamati ya Nidhamu TFF
Yondani anakabiliwa na kosa la kinidhamu la kumtemea mate beki wa Simba, Asante Kwasi kwenye mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
BEKI wa Yanga, Kelvin Yondani 'Vidic' ameigomea kamati ya nidhamu iliyomwita kabla ya kutoa maamuzi ya utovu wa nidhamu aliyoufanya kwenye mchezo wa watani wa jadi, Aprili 29.
Yondani anakabiliwa na kosa la kinidhamu la kumtemea mate beki wa Simba, Asante Kwasi kwenye mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kutohudhuria kwa Yondani kwenye kikao hicho, Afisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa hawana taarifa zozote kutoka kwa mchezaji husika ambaye ameshindwa kuitikiwa wito wa kamati ya nidhamu.
"Kamati inawajibika kutuma tena barua kwa mchezaji huyo wa Yanga kwa mara ya mwisho na kama asipotokea inamaana kamati itasikiliza upande mwingine na kutoa maamuzi," alisema Ndimbo.
Kutokana na kosa hilo Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) ilimsimamisha Yondan na suala lake likipelekwa kwa kamati ya nidhamu ambayo ipo kwenye mchakato wa kumchukulia hatua beki huyo.
Pia Kamati ya nidhamu imetoa hukumu kwa mchezaji wa Mbeya City, Ramadhani Malima ambeye aliingia uwanjani na kushangilia na wenzake kwenye mechi dhidi ya Yanga,Aprili 22 wakati huo akiwa ameonyeshwa kadi nyekundi.
Malima ametiwa hatia kwa kanuni ya 37 kifungu cha saba ambapo atafungiwa mechi tatu na kulipa faini ya laki tano, kutokana na kukosa kwake mchezo mmoja uliopita kwa hivyo atatumikia adhabu ya mechi mbili.
source Mwanasport
No comments