Breaking News

NINJE ATAKA NYOMI LA MASHABIKI TAIFA

Ninje amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani hapo kwani anaamini nyomi la watakaojitokeza litawahamasisha vijana wake kupata matokeo mazuri.

NGORONGORO Heroes keshokutwa Jumapili inatarajiwa kuikaribisha Mali katika mechi yao ya mkondo wa kwanza wa kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana wa umri chini ya miaka 20, huku kocha wake, Ammy Ninje, akiita mashabiki wajae Uwanja wa Taifa.

Ninje amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani hapo kwani anaamini nyomi la watakaojitokeza litawahamasisha vijana wake kupata matokeo mazuri.

“Mashabiki ni muhimu, ni sawa na mchezaji wa 12 uwanjani, wanapojitokeza kwa wingi vijana wanapata moyo kuona wana thamani kama ilivyo Taifa Stars, hivyo naomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili waiunge mkono timu yao,” alisema Ninje.

Kuhusu maandalizi yao, Kocha Ninje alisema wachezaji wapo fiti na ameijenga saikolojia ya wachezaji ili kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani ili wakienda ugenini kazi isiwe kubwa.
“Tunaposhinda nyumbani jambo la kwanza itatujengea ujasiri wa kupambana ugenini na tunakuwa na plani ya kulinda matokeo yetu na ndio maana tunaona umuhimu wa kufanya kila jambo ili tupate matokeo,” alisema.
Ngorongoro itarudiana na Mali wiki ijayo na kama itafuzu kutinga raundi ya tatu itavaana na mshindi kati ya Uganda na Cameroon kuwania kusonga mbele.

No comments