MAPOKEZI YA SIMBASC ZANZIBAR HAYANA MBWEMBWE
Simba ndiyo walianza kuingia visiwani Unguja leo Jumatano mchana na kufuatiwa na watani zao Yanga walioingia jioni.
Lakini mapokezi ya timu hizo yalikuwa tofauti ambapo Yanga ilionyesha kuwa na mashabiki wengi kutokana na jinsi walivyojitokeza kuwapokea kwenye bandari ya Unguja.
Baada ya kutua na kuingia kwenye gari lao lililoandaliwa na waratibu wa mashindano hayo waliongozwa na msafara wa gari la wazi nyuma maarufu kama kirukuu lililobeba mashabiki wao.
Hata hivyo, kikosi cha Yanga pamoja na kupokelewa kwa mbwembwe bado mashabiki waliokuwepo hapo walitamani kuwaona nyota wao kama Harieter Makambi ambaye anaongoza kwa mabao kiti ya Bara akiwa na mabao 11.
Tofauti ni nyingine iliyojitokeza kwa timu hizo ni pale ambapo nyota wa Simba waligombewa kupiga picha na mashabiki kuliko nyota wa Yanga hata wale ambao wapo kikosi cha kwanza waliokuja kuongeza nguvu kama Deus Kaseke, Haji Mwinyi
No comments