Breaking News

SIMBA YANGA ZAMPASUA KICHWA KOCHA

Biashara ambayo ndio msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu,haijawa na mwenendo mzuri kwani kati ya mechi 17 ilizocheza imeshinda moja,sare saba na kupoteza tisa ambapo ipo mkiani kwa alama 10.

MWANZA. BAADA ya kusaini kandarasi ya miezi sita kuitumikia Biashara United, Kocha Amri Said ‘Stam’ ameweka wazi mikakati yake kuwa ni kuhakikisha anainusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja.

Kocha Stam alitangazwa juzi Jumanne na Uongozi wa  klabu hiyo kuchukua mikoba ya aliyekuwa Kocha Mkuu raia wa Rwanda, Hitimana Thiery ambaye alivunja mkataba na Chama hilo la mkoani Mara.

Biashara ambayo ndio msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu,haijawa na mwenendo mzuri kwani kati ya mechi 17 ilizocheza imeshinda moja, sare saba na kupoteza tisa ambapo ipo mkiani kwa alama 10.

Akizungumza na Mwanaspoti, Stam alisema kuwa moja ya mikakati yake kwanza ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kuitoa mkiani na kuinusuru kushuka Daraja na kwamba anaamini kwa uwezo atafanya vizuri.

Alisema kuwa zipo timu nyingi ambazo zilihitaji huduma yake,lakini ameamua kujiunga na Biashara United ili kudhihirisha ubora wake katika kufundisha soka na kwamba kikubwa ni ushirikiano ndani ya klabu.

“Kwanza kabisa nataka kuitoa timu mkiani baada ya hapo niinusuru kushuka Daraja,najiamini sana kwenye kazi hii,kikubwa niwaombe mashabiki ushirikiano,timu nyingi zilinihitaji lakini nimeamua nije huku ili nilete kitu kipya”alisema Stam.

Hata hivyo Kocha huyo alifafanua kuwa ameamua kufanya kazi na Msaidizi wake Omary Madenge anayelingana naye kiwango cha elimu (Leseni B) kutokana na muda mrefu alionao kwenye timu.

“Ni kweli Msaidizi wangu tunalingana kiwango cha elimu,lakini nimepewa majukumu niamue kumuacha au kumbakiza,lakini nimeona niendelee naye kwakuwa yeye ana muda mrefu kwenye timu hivyo atanisaidia baadhi ya mambo”alisema Kocha huyo.

Ligi hiyo inaongozwa na Yanga yenye alama 50 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao 33.

No comments