TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO 2,2,2019
Inter Milan wanamnyatia beki kamili wa Manchester United Ashley Young, 33, na wanatumai kwamba wataweza kumchukua bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu baada ya mkataba wake kumalizika. (Mirror)
Meneja Unai Emery amesema Arsenal bado hawajazungumzia uwezekano wa kumnunua beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill, 33, Januari. (Football.London)
Lakini meneja wa Fulham Claudio Ranieri amekuwa wakimtaka Cahill akitumai kumtumia kuimarisha safu yake ya ulinzi Craven Cottage. Anamtaka kwa mkopo wa miezi sita. (The Sun)
Emery amefahamishwa kwamba Arsenal hawataunga mkono mpango wake wa kutaka kuwarejesha Calum Chambers, 23, na Reiss Nelson, 19, mwezi huu. Wawili hao wako nje kwa mkopo. (Metro)
Gary Cahill Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gary Cahill
Chelsea wanakariiba sana kukamilisha usajili wa kiungo wa kati Mmarekani Christian Pulisic, 20, kwa £45m kutoka Borussia Dortmund. (Express)
Monaco wanapanga kukamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas, 31, mwezi huu wa Januari, hatua ambayo itamkutanisha na mchezaji mwenzake wa zamani Arsenal Thierry Henry ambaye sasa ni meneja. (Daily Mail)
Cesc Fabregas Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cesc Fabregas
Mkufunzi mkuu wa Chelsea Maurizio Sarri amesisitiza kwamba hahitaji kununua mshambuliaji mwingine Januari hata kama jeraha la kifundo cha mguu linalomtatiza Olivier Giroud litazidi. (ESPN)
West Ham wanapanga kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Everton James McCarthy, 28, kama sehemu ya mpango wao wa kuimarisha kikosi chao Januari. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, hataki kuitwa arejee katika klabu hiyo kwa sababu anafurahia maisha yake kwa Aston Villa kwa mkopo, anasema meneja Dean Smith. (Sky Sports)
Tammy Abraham in action for Aston Villa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tammy Abraham
Lakini Wolves wanaongoza kinyang'anyiro cha kutaka saini ya Abraham, ambaye amewafungia Villa mabao 16 msimu huu. (Daily Mail)
Tottenham wako radhi kumtuma George-Kevin Nkoudou, 23, nje kwa mkopo Januari. (Footmercato)
Bora kutoka Jumanne
Pogba akicheza kusherehekea bao lake la kwanza mechi dhidi ya AFC Bournemouth ambapo walishinda 4-1. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pogba akicheza kusherehekea bao lake la kwanza mechi dhidi ya AFC Bournemouth ambapo walishinda 4-1.
Kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil, 30, amesema hataihama klabu yake ya Arsenal kwa mkopo mwezi huu wa Januari. Badala yake, amesema yuko tayari kusalia kupigania nafasi yake katika kikosi. (ESPN)
Juventus wamewasilisha ofa kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 28, ambapo wanataka kumpa mkataba wa miaka minne ambapo atakuwa analipwa £138,000 kila wiki. (Tuttosport kupitia The Sun)
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anawakosea heshima wapinzani wake kwa jinsi anavyosherehekea kufunga mabao, hilo kwa mujibu wa kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Claude Makelele. Pogba amekuwa akisherehekea kufunga mabao kwa kucheza ngoma, lakini Makelele anaamini amevuka mipaka. "Inaudhi sana. Namshauri Pogba. Nataka kumwambia, 'Sikiliza, nenda kama hivyo katika chumba cha kubadilishia mavazi, sio sasa [uwanjani]. Inaudhi sana. Mnashinda 4-0, kisha unacheza ngoma hapa mbele yangu," amesema Makelele (Daily Mirror)
Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot hana mpango wowote wa kuhamia Tottenham kwa sababu anaichukulia klabu hiyo kuwa ya chini ya kiwango chake kama mchezaji. Mchezaji huyo wa miaka 23 hata hivyo bado anataka kuihama PSG. (ESPN)
Mwenyekiti na mmiliki wa Huddersfield Dean Hoyle hana nia ya kuiacha klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England iendeleze kuteleza na kushushwa daraja na ameahidi kuwanunua wachezaji zaidi Januari. (Daily Mail)
No comments