Breaking News

YANGA WATOA TAMKO KUHUSIANA NA SIMBA KUCHAPWA CAF, USHIRIKINA WATAJWA


By Godfrey Godstar,

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameuzungumzia mchezo wa AS Vita dhidi ya Simba ambao ulimalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 5-0.

Taarifa imeelezwa Zahera amefunguka kwa kusema Simba walifungwa kutokana na kuweka mbele imani za kishirikina badala ya kujipanga kupambana uwanjani.

Amesema Simba walikuwa na wachezaji wote wazuri lakini walishindwa kufuata maelekezo waliyopewa mazoezini na kusababisha kufungwa idadi hiyo ya mabao.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amesema kitendo cha Simba kuamini ushirikina ikiwemo suala la kutoka hoteli moja kwenda nyingine limesababisha waweze kuvurunda.

Amekiongelea kitendo hicho cha kuhama ni kama ushirikina kwani hakijasaidia lolote na badala yake wakapoteza kirahisi huku akisema wapinzani wao waliwazidi kila idara.

No comments