YANGA YAPEWA ONYO
By Godfrey Godstar,
Baada ya kufanikisha kuichapa bao 1-0 juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali 'Bilo', amewaambia Yanga hakuna timu yenye uhakika na ubingwa kwa sasa.
Bilo amesema ukiangalia Yanga kwa sasa licha ya kuwa ipo kileleni, bado haina nafasi ya kuchukua ubingwa kutokana na watani zake wa jadi kuwa nyuma kwa mechi nyingi.
Aidha, Bilo amewataja pia Azam kuwa na mwendelezo mzuri akiamini yoyote yule atayayezidi kufanya vizuri atafanikiwa kubeba taji.
Katika msimamo wa ligi unaonesha kuwa Yanga ambao wamecheza mechi 20 wako kileleni wakiwa na alama 53.
Vilevile Simba ambao wako nyuma dhidi ya Yanga kwa alama 20, mpaka sasa wamecheza jumla ya mechi 14 pekee.
No comments